Hii ni kulingana na hesabu ya chuo kikuu cha Johns Hopkins, hapa Marekani.
Marekani inaongoza kote duniani kwa idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona na vifo.
Jumla ya watu milioni 18 wamethibitishwa kuambukizwa Corona kufikia jumatatu jioni, na zaidi ya 319,000 kufariki.
Maambukizi yameongezeka katika jimbo la California siku chache baada ya sikukuu ya Thanksgiving.
Kufikia sasa, watu milioni 1.9 wameambukizwa corona na 22,000 kufariki kutokana na virusi hivyo katika jimbo la Carlifonia. Watu kadhaa wanaambukizwa kila siku.
Gavana wa jimbo hilo Gavin Newsom, ameonya kwamba hali ya maambukizi inaendelea kuwa mbaya sana, na kuwataka wakaazi kuheshimu maagizo ya maafisa wa afya.
Amesema kwamba amri aliyotangaza ya watu kusalia nyumbani kwao ili kudhibithi maambukizi, huenda ikaendelea kutumika.
Huu ndio mwaka katika historia ya Marekani, ambapo imerekodi idadi ya juu sana ya vifo, hasa kutokana na virusi vya Corona.
Wataalam wanasema kwamba huenda zaidi ya watu milioni 3 wakafariki mwaka huu.
Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC