Watu 4000 wanakimbilia Sudan kila siku kutoka Ethiopia kutokana na mapigano Tigray

Raia wa Ethiopia wanaokimbilia Sudan

Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi – UNHCR, limesema kwamba zaidi ya wakimbizi 27,000 wamekimbia kutoka Ethiopia na kuingia mashariki mwa Sudan, kufuatia mapigano yanayoendelea eneo la Tigray.

Wanasema kwamba idadi hiyo ya wakimbizi ni kubwa zaidi kuwahi kuoekana katika siku za hivi karibuni nchini Sudan.

Kwa kiwango cha wastani, wanawake, Watoto na wanaumme 4,000 wanavuka mpaka wa Ethiopia na kuingia Sudan kila siku.

Hali imeendelea kuwa mbaya katika eneo la Tigray tangu serikali ya Ethiopia ilipoanza mashambulizi ya kijeshi wiki mbili zilizopita.

Serikali ya Ethiopia imesema mashambulizi hayo yanatokana na shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa Tigray – TPL dhidi ya kambi ya jeshi la serikali.

Maafisa wa UNHCR wamesema kwamba hali ya kibinadamu inaendelea kuwa mbaya katika eneo la Tigray.