Trump na Biden wakutana kwa mdahalo wa kwanza Jumanne

Jukwa la mdahalo wa kwanza kati ya Rais Donald Trump na mgombea wa chama cha Democratic, makamu rais wa zamani Joe Biden mjini Cleveland, Ohio, U.S. Septemba 28, 2020. REUTERS/Jona

Wamarekani kwa mara ya kwanza wataweza kuwaona wagombea wawili wa kiti cha rais wanaoshindana vikali wakijadilia juu ya masuala muhimu ya taifa kwenye jukwa moja kwa mdahalo wa kwanza kati ya tatu.

Wachambuzi wengi hata hivyo wanasema hawamini mdahalo huo utaweza kubadili mawazo ya wapiga kura ambao wameshamua ni nani watampigia kura na ni wachache sana ambao hawajaamua bado.

Trump mwenye umri wa miaka 74 na Biden miaka 77 wanakutana mbele ya idadi ndogo ya watu kutokana na masharti ya Covid 19 baada ya kushambuliana vikali hivi karibuni juu ya uwezo wao wa kutumikia kiti cha rais, Trump akidai Biden anatumia dawa za kumpatia nguvu na anahitaji kupimwa.

Joe Biden, kushoto na Donald Trump kulia wako tayari kwa mdahalo

Biden akijibu kwamba Trump ni kiongozi hatari ambae hakuchukua hatua zinazostahiki kupambana na janga la corona, uchumi na ubaguzi wa rangi hapa nchini, na atakta havari zaidi kwa usalama wa taifa.

Trump kwa hivyo anaingia uwanjani tayari kujitetea, akiwa yuko nyuma mpinzani wake katika utafiti wa maoni kitaifa. Huku Biden akingia uwanjani akiwa na matumaini ya kubadili maoni ya wale ambao bado hawajamua.

Joe Rosky anajitaja kua ni mdemokrat wa Ohio na alimpigia kura Trump katika uchaguzi wa 2016.

"Lakini kwa wakati huu, kwa hakika sijui nitampigia kura nani, ninachojua nitakwenda kupiga kura. Kama nilivyosema safari ya mwisho nilimpigia Trump. Sijui nitafanya nini safari hii, itanibidi kuchunguza vyema kuhusu Biden na kuona kama nina kubaliana na mawazo yake ndipo niamuwe," amesema Rosky.

Ohio ni moja kati ya majimbo manane yenye ushindani ambayo ni lazima mgombea apate ushindi kuweza kunyakua ushindi hapo Novemba 3 2020.

Biden anaongoza katika majimbo hayo yenye ushindani mkali kulingani na utafiti wa maoni wa karibuni unaofanywa na taasisi mbali mbali.

Katika majimbo hayo mvutano ni mkali hadi kusababisha majirani na familia kutengana kama Patty Lucci anaemunga mkono Biden alivyoiambia Sauti ya Amerika.

"Nusu ya watoto wangu ni wafuasi wa Trump. Kwa hivyo hatuwaaliki tena hapa nyumbani (laughs) hadi mwakani. Tulisema hatutazungumza kuhusu siasa tena, lakini tunajikuta tunazungumzia siasa. Na mwishowe tukawazuia kuja,"

Waandamanaji wa vuguvugu la Black Lives Matter mjini Portland, Ore. Aug. 2, 2020.

Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi na unyanyasaji wa polisi dhidi ya watu weusi yamezusha wasi wasi miongoni mwa wafuasi wa Trump na ni suala linalotazamiwa kujadiliwa kwa kina waakt wa mdahalo wa Jumanne. Dolores Gentile mfuasi wa Trump anasema wamekua na hofu kutokana na jinsi suala hilo limeligawa taifa hata kuogopa kuweka bange la Trump nej ya nyumba Lake.

"Nilijiuliza kwa muda ikiwa niweke bango la Trump nje ya nyumba yangu au la kwa sababu niliogopa huwenda nyumba yangu ikafyetuliwa risasi . Na baadae nikafikiria, na kusema unajua nini siwezi kukubali kuishi kwa hofu," amesema Gentile.

Ingawa Biden anakwenda kwenye mdahalo akiwa na nguvu hasa baada ya gazeti la New York Times kuchapisha ripoti kwamba Trump alilipa kodi chache na kuendelea kutilia shaka upigaji kura kwa njia ya posta anabidi kuwavutia wale ambao hawajamua bado na kusisitiza juu ya utendaji kazi wa trump kuhusiana na janga la corona.

Huku Trump anaelekea Cleveland akiwa anaongoza upande wa suala la uchumi na licha ya matatizo yote yanyao mkabili yungali anaungwa mkono na wafuasi wake sugu akiwapatia nguvu kwa kumteua jaji mhafidhina Amy Coney Barrett kuchukua nafasi ya jaji shuja wa mengo wa kushoto Ruth Bader Ginsburg anaezikwa wiki hii hii.