Boustani alipatikana hana hatia baada ya a kesi iliyosikilizwa kwa wiki sita kuhusiana na tuhuma za ubadhirifu wa dola blioni 2 ikiwa ni pigo kubwa kwa waendesha mashtaka wa serikaloi ya marekani.
Boustani anafaniya kazi kampuni ya ujenzi wa meli ya dubai ya Privinvest. Na kati ya 2013 na 2014 makampuni ya usalama yanayomilikiwa na Msumbiji yalichukua mkopo wa dola bilioni 2 kutoka benki za Uswisi Credit Swiss na VTB ya Rashia, ili kununua meli za kijeshi na uvuvi kutoka Privinest. Lakini serikali ilpolitangaza deni hilo mwaka 2016, taifa hilo maskini la kusini mwa Afrika lilitumbukia katika mzozo mkubwa wa kifedha. Marekani inadai kwamba angalau dola milioni 200 ya mkopo huo ziliztumiwa kuwahonga wanasiasa na maafisa wa vyeo vya juu wa serikali.
Boustani alikiri aliwalipa mamilioni ya dola maafisa wa Msumbiji kwa ajili ya kupata kandarasi ya vifaa hivyo lakini, anasisitiza kwamba ilikuwa malipo ya halali na wala si mrungura.
Bostani alikamatwa mwezi januari katika Jamhuri ya Dominica na kusafirishwa hadi Marekani.
Katika ushahidi wake mfanyabaishara huyo alidai kwamba sehemu ya fedha hizo zilitumiwa kugharimia kampeni ya rais Filipe Nyusi mwaka 2014.
Fedha zilitolewa wakati Nyusi alikua waziri wa Ulinzi. Alishinda katika uchaguzi huo na akachaguliwa tena mwaka 2019.
Waendesha mashtaka wa Marekani walichukua kesi hiyo kwa sababu deni hilo ambalo halikulipwa liliuziwa wawekezaji wa Marekani.
Waendesha mashtaka wamesema wawekezaji walidanganywa bila ya kuelezwa njama ya rushwa iliyokuwepo kuhusiana na mkopo huo.
Mkopo ulipotangazwa mwaka 2015 Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, lilisitisha msaada wake kwa Msumbiji na sarafu kuporomoka mara moja.
Chama tawala cha Msumbiji FRELIMO kinakanusha kwamba Nyusi alifanya kosa lolote lakini chama kikuu cha upinzani RENAMO kimemtaka ajiuzulu.
Washirika watatu wa Boustani walikiri mapema kwamba wanahatia.