Watu 150 waokolewa saa 16 baada ya shambulizi katika hoteli mjini Nairobi

Maafisa wsa Usalama wa Kenya wakiwasaidia watu kutoka nje ya hoteli ya DusitD2 Nairobi, Kenya, hapo January 15, 2019.

Wakazi wa Nairobi waamka asubuhi ya Jumatano wakiambiwa kwamba kungali na watu walokwama ndani ya majengo ya hoteli ya kifahari na afisi mbali mbali, saa 16 baada ya kushambuliwa na washambulizi wanaodhaniwa ni wa kundi la al-Shabab.

Kundi hilo la wapiganaji wa kisomali wa itikadi kali limedai kuhusika na shambulio hilo lililotokea Jumanne mchana na kusababisha vifo vya watu 15 na idadi ya wajeruhi wasojulikana.

Milio ya bundukina milipuko iliendelea kusikika alfajiri saa 12 baada ya shambulizi kutokea katika mtaa wa kifahari wa Riverside Drive, na hivyo kutofautiana na maelezo ya polisi wa Kenya kwamba wamedhibiti hali ya mambo huko.

Karibu watu 150 waliokolewa kiasi ya saa tisa asubuhi na kukiwa na ripoti ya mamia wengine wangali wamejificha sehemu mbali mbali ya majengo hayo.

Your browser doesn’t support HTML5

Watu 150 waokolewa asubuhi baada ya shambulizi la hoteli ya DusitD2 Nairobi