Jacob Zuma ahusishwa na Russia katika mikataba ya ufisadi

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma katika uwanja wa Mahakama Kuu huko Durban, Afrika Kusini,April 6, 2018.

Waziri wa fedha wa Afrika kusini Nihilanihila Nene ameeambia jopo la wachunguzi kuhusiana na kashfa za ufisadi dhidi ya aliyekuwa rais Jacob Zuma, kwamba alifutwa kazi na Zuma baada ya kukataa kuidhinisha mkataba baina ya Russia na Afrika kusini, wa kiasi cha dola bilioni 100, mwaka 2015.

Nene ni afisa wa ngazi ya juu kutoa ushahidi dhidi ya Jacob Zuma katika kesi ya ufisadi ambayo pia unahusu familia ya Gupta, marafiki wa Zuma wanaoshutumiwa kwa kutumia uhusiano wao wa karibu na Zuma kupata zabuni za thamani kubwa ya fedha kutoka serikalini.

Zuma amekana madai kwamba aliingia mkataba na rais wa Russia Vladmir Putin wakati wa mkutano wa BRICS, wa kujenga silaha za nuclear.