Pompeo kukutana na Kim kuhusu nuclear

Pompeo

Waziri wa mambo ya nje wa marekani Mike Pompeo anatarajiwa kurejea Pyongyang jumapili oktoba 7, kwa mazungumzo na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya marekani - Heather Nauert – amesema kwamba mazungumzo kati ya Pompeo na Kim, yataangazia jinsi ya kumaliza utengenezaji wa silaja za nuclear.

Nauer amesema kwamba marekani haijabadili sera zake na itatekeleza hatua ya kuiwekea vikwazo Korea kaskazini iwapo haitaacha utengenezaji wa silaha za nuclear.

Lakini msemaji wa Korea kaskazini Ri Yong Ho, aliambia baraza la umoja wa mataifa wiki jana kwamba vitisho vya vikwazo dhidi ya Korea kaskazini vinaweka mazingira ya ukosefu wa uaminifu na marekani, hatua ambayo inaifanya Korea kaskazini kusita kuharibu silaha zake za nuclear kabisa.