Mahakama yataka Marekani kuondoa vikwazo vya Iran

Mahakama ya juu ya umoja wa mataifa imeamurisha marekani kuondoa vikwazo ilivyoiwekea Iran kuhusiana na madawa, chakula na vifaa vya kutengeneza ndege.

Hatua ya mahakama ya umoja wa mataifa ndio ya hivi punde katika kesi dhidi ta vikwazo vilivyotolewa na rais wa marekani Donald Trump dhidi ya Iran mapema mwaka huu.

Iran imelalamikia mahakama ya kimataifa kuhusu hatua ya marekani kuiwekea tena vikwazo vilivyokuwa vimefutiliwa mbali, chini ya mkataba wa kimataifa wa nuclear wa mwaka 2015.

Katika uamuzi wake, jaji wa mahakama ya kimataifa - Abdulqawi Ahmed Yusuf - amesema kwamba vikwazo vya marekani dhidi ya Iran, ambavyo viliwekwa mwezi Mei, vinaweza kuhatarisha usalama wa safari za anga za Iran.