Kuchora kibonzo cha rais Kagame ni kosa la jinai Rwanda

Rais wa Rwanda Paul Kagame

Serikali ya Rwanda imetunga sheria inayomzzuia mtu yeyote kuchora kibonzo cha rais wa nchi hiyo Paul Kagame au kiongozi yeyote wa ngazi ya juu.

Anayekiuka cheria hiyo, atafunguliwa makosa ya jinai ambayo adabu yake ni kifungo cha maisha.

Sheria hiyo imesababisha wasiwasi kati ya waandishi wa habari nchini Rwanda wanaohisi kwamba hilo itatatiza utendaji kazi wao

Kwa mujibu wa sheria hii kuchora katuni na kuonyesha viongozi wa ngazi za juu akiwemo Rais wa nchi inayoweza kutafsiriwa kama hatua ya kumchafulia jina litakuwa ni kosa la jinai.

Waandishi wa habari wanahisi kwamba sheria hiyo inalenga kuwanyima uhuru wao wa kuasilisha habari kwa uma kupitia kwa michoro.

Hata hivyo waziri wa sheria ambaye pia ndiye mwanasheria mkuu wa serikali Johnston Busingye ameonekana kutetea hatua ya serikali, akidai kwamba hilo halipaswi kuwapa wasiwasi wadau katika sekta ya habari nchini Rwanda.

“Kipengele kizima cha kashfa au kuchafua jina la mtu ktk sheria zetu za jinai kimeondolewa nimesema tu vimesalia vijisehemu viwili tu kuhusu uchoraji katuni na nimefafanua kwa undani kwamba navyo vinasubiri wakati wake na labda nifafanue zaidi tangu nimekuwa kwenye sekta hii ya sheria kwa miaka hiyo yote kamwe sijawahi kuona mtu aliyefikishwa kizimbani kwa shutuma za kuchora katuni” amesema waziri Busingye.

Mabadiliko mengine makubwa kwenye sheria hiyo ni kwamba tofauti na hapo awali, Daktari atakuwa na mamlaka ya kuavia mimba ikiwa itabainika sababu za msingi zinazoonyesha mimba hiyo itaweza kuwa hatari kwa mama.

“Mtu anamaliza miezi sita mahakamani na baada ya hapo inaonekana si rahisi kuitoa mimba hii au inampa shida kwenda mahakamani kudai apewe idhini ya kuavia mimba haya yote yameondoka itakuwa ni kati yake na daktari wake” ameendelea kusema Busingye

Hata ivyo wengi wanahisi hii inaweza kuendekeza watu kutoa mimba ovyo vyo kwakuwa sasa yaonekana kuwa rahisi.Lakini baadhi ya madaktari pia wamepuuza hilo wakisema bado jicho la sheria kujua uhalisia wa kutoa mimba litaendelea kuwa kali.

Imetayarishwa na Sylivanus Karemera, sauti ya Amerika, Kigali, Rwanda.