Tillerson aondolewa kama Waziri wa Mambo ya Nje Marekani

Mike Pompeo

Ikulu ya Marekani, White House, imetangaza kwamba Rais Donald Trump amemwondoa waziri wake wa mambo ya nchi za nje Rex Tillerson na kumchagua mkurugenzi wa idara ya ujasusi ya CIA, Mike Pompeo kuchukua nafasi yake.

Nafasi ya Pompeo katika CIA itachukuliwa na aliyekua naibu wake Gina Haspel, mwanamke wa kwanza kuchukua wadhifa huo.

Katika ujumbe wa twitter, Rais Trump alimshukuru Tillerson akisema, "Mike Pompeo, Mkurugenzi wa CIA atakua waziri mpya wa mambo ya kigeni. Atafanya kazi nzuri kabisa. Ahsante Rex Tillerson kwa huduma yako! Gina Haspel atakua mkurugeni mpya wa CIA na anakua mwanamke wa kwanza kuteuliwa kwa kazi hiyo. Hongera kwa wotre."

Wachambuzi wanasema ingawa ni habari kubwa lakini ilikua inatarajiwa kutokana na hali ya kutoelewana kati ya Trump na Tillerson ambao hawakua na msimamo moja katika sera na Tillerson kutoa mara kadhaa matamshi yaliyokua tofauti na msimamo wa Trump.