Wanawake washiriki katika miradi ya Sayansi, Teknolojia

Your browser doesn’t support HTML5

Wasichana mbali mbali hivi sasa nchini Kenya, wanajishughulisha na miradi ya sayansi na teknolojia kama njia ya kutatua changamoto mbali mbali katika jamii. Mradi maarufu wa Tech Women ambao ulianzishwa na serikali ya Marekani kusaidia wanawake barani Afrika, Asia na Mashariki ya kati umepokelewa vyema nchini Kenya na hivi sasa unaonekana kuwa unazaa matunda. Wasichana mbali mbali waliojiunga na mradi huo tayari wameanza kushirikiana katika kubaini na kutatua matatizo yanayokumba maeneo yao na kuanza kuyatatua kwa kutumia elimu ya sayansi. Mwandishi Salma Mohammed anaripoti zaidi kutoka Mombasa