Vikwazo hivyo ambavyo vimesitisha uingizaji wa bidhaa muhimu nchini Yemen, na kuonya kwamba maisha ya maelfu ya watu yako hatarini.
Viongozi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Shirika la Afya duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), walisema katika taarifa ya pamoja Ijumaa, kwamba gharama ya vikwazo hivyo inapimwa kwa idadi ya watu waliopoteza maisha yao.
Aidha mashirika hayo yamesema kuwa takriban watu milioni saba wako katika hatari ya kufa njaa nchini Yemen, na idadi hiyo huenda ikaongezeka na kufikia Zaidi ya milioni tatu. Taarifa hiyo imeeleza mzozo huo kama ni mgogoro uliokuwa mbaya zaidi duniani.
Wiki iliyopita, muungano huo udhibitinjia za angani, ardhini na maji, kuingia Yemen, kufuatia shambulizi la kombora, lililotekelezwa na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran, karibu na mji mkuu wa Riyadh.