Waandamanaji wa mungano wa upinzani NASA wanataka maafisa waandamizi wa tume hiyo waloshtumiwa kuhusika na kasoro zilizotokea wakati wa uchaguzi wa Ogusti 8 washtakiwe kabla ya kufanyika kwa marudio ya uchaguzi wa rais.
Baada ya kufukuzwa kutoka ofisi za IEBC wafuasi hao walikusanyika katika sehemu nyingine za Nairobi na polisi waliwafuata na kufyetua mabomu zaidi ya kutoa machozi.
Kiongozi wa Upinzani mgombea kiti cha rais Raila Odinga alikutana na waandishi habari hii leo na kutaka mageuzi yafanyike ndani ya tume ya uchaguzi kabla ya uchaguzi kufanyika.
Ni wazi kabisa IEBC haina nia ya kufanya mageuzi ili iweze kuwa taasisi ya uchaguzi ya kuaminika, inaridhia sana matakwa ya Jubilee kuweza kuanza utaratibu huo . kwa vyevyote vile IEBC haiwezi kuanza utaratibu wa kuhakikisha uchaguzi wa haki wakati wale walowajibika na karosa na makosa ya kisheria wangali wanaingia na kutoka katika afisi za IEBC na wamekata kuwafukuza. Na ndio maana hii leo tunaanza kampeni kwa njia yaAmani kuwahimiza kuanzisha utaratibu wa haki wa uchaguzi.
Kiongozi huyo amesema hatoshirika katika uchaguzi wa marudio hadi pale maafisa hao wamefukuzwa na kuhukumiwa.
Usalama umeimarisha katika mji mkuu wa Nairobi ambapo polisi wa kupambana na ghasia wamewekwa katika sehemu muhimu za mji huo.
Your browser doesn’t support HTML5
Wakati huo huo, wafuasi wa chama kinachotawala cha Jubilee, na wanaomuunga mkono rais Uhuru Kenyatta, pia waliandamana, wakitaka kusifanyika mabadiliko yoyote kwenye tume hiyo. Mahakama ya juu ilibatilisha matokeo ya uchaguzi huo kama yalivyotangazwa na IEBC, na kusema kuwa zoezi hilo liligubikwa na dosari. Iliamuru uchaguzi huo urudiwe ndani ya kipindi cha siku 60.
Tume ya IEBC imetangaza kuwa uchaguzi wa matrudio utafanyika tarehe 26 mwezi ujao. Wakati huo huo, kiongozi wa upinzani Raila Odinga, leo amesema kuwa serikali imeondoa maafisa wa kulinda usaloama wake pamoja na wale wa kulinda usalama wa mgombea wake mwenza, Kalonzo Musyoka. Odinga amesema hayo alipowahutubia waandishi wa habari mjini Nairobi leo alasiri.