Kenya yawezesha wananchi kujipima HIV kwa siri

Kifaa maalum cha mtu kupima HIV mwenyewe

Kenya imekuwa mstari wa mbele katika nchi za Kiafrika hivi karibuni kuwezesha upatikanaji wa vifaa maalum vya mtu kujipima mwenyewe HIV katika juhudi za kuhamasisha watu wengi zaidi kujua hali zao na kutafuta matibabu.

Serikali inakadiria kuwa kuna watu wanaofikia nusu milioni Kenya ambao wana virusi vya HIV lakini hawajitambui.

Kijana mwenye umri wa miaka 25, Lucy Wanjiku amepata habari ya kifaa hiki cha kupimia na ameamua kujaribu kukitumia.

Vifaa hivyo vya kujipima mwenyewe vilianza kuuzwa kwa bei nafuu katika maduka ya madawa tangia mwezi Mei.

Mfamasia kwanza humuelezea anaye nunua namna ya kukitumia kifaa hicho, uwezekano wa matokeo ya vipimo na taarifa juu ya kuwasiliana na hospitali za rufaa kabla ya kukitumia kifaa hicho.

Kwa mujibu wa Wanjiku, kifaa hicho cha kujipima mwenyewe kitasaidia kupunguza unyanyapaaji.

“Kwa kuwa mtu anakitumia mwenye kwa faragha, hapana atakaye kiona. Sifikirii kuwa kuna unyanyapaaji mkubwa kwa hilo na pia, kama ilivyokuwa mfamasia hatopata kuona majibu ya vipimo vyangu pia hawatojua kama majibu yangu ni chanya au hasi. Hiyo ni siri yangu mwenyewe.”

Kuna aina mbili za vipimo katika kifaa hiki cha kujipima mwenyewe- kiko kile cha kuweka mdomoni na kingine ni kipimo cha damu.

Kifaa cha kuchukua damu kina chupa tatu ambazo zinawezesha kutenganisha damu kwa haraka. Pia inakifuko cha kuhifadhia kifaa cha kuchukua kipimo na sindano ya kutolea damu.

Kipimo cha kupima damu kinauzwa dola za Marekani 8.00 (shilingi za Kenya 850) wakati kifaa cha kupimia mdomoni kinauzwa rejareja dola 9.00( KES 950).

Serikali tayari imekwisha wapa mafunzo wafamasia kama vile Dr Miriam Mugure kusimamia upimaji huo.