Wafaransa wawachagua wanasiasa wapya kugombania kiti cha rais

Emmanuel Macron mshindi wa duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais akiwapungia mkono wafuasi wake.mjini Paris, France, April 23, 2017.

Matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa yamethibitishwa kwamba mgombea wa mrengo wa kati asiye na chama Emmanuel Macron na mgombea mzalendo anayepinga wahamiaji Marine Le Pen ndio washindi wa duru ya nkwanza.

Wagombea hao hivi sasa watashindana katika duru ya pili May 7, katika kile wachambuzi wanasema kimesababisha mtikisiko mkubwa wa kisiasa nchini Ufaransa.

Itakua mara ya kwanza kwa Ufaransa kua na uchaguzi wa rais bila ya wagombea kutoka vyama vikuu vya muda mrefu, na kuleta utata kwa wanasiasa wakongwe na kuwa jambo litakalo amua kama Ufaransa itataka kubaki ndani ya Umoja wa Ulaya EU ama kufuata njia ya Uingereza kujitoa kutoka EU, na ya Marekani kumchagua Donald Trump.

Wafuasi wa Le Pen wakisherehekea ushindi wake

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Paris Mohamed Saleh anasema “ni mabadiliko makubwa katika sisa za Ufaransa kwani tangu utawala wa Charles de Gaulle zaidi ya miaka 40 iliyopita hakutakuwepo na mgombea wa vyama vikuu vya mreengo wa kushoto wale kulia katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais.”

Your browser doesn’t support HTML5

Uchaguzi wa kihistoria wa Ufaransa na Mohamed Saleh

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa, Macron amepata asilimia 23.8 huku Le Pen akipata asilimia 22 za kura wakiwaacha wagombea wengine 9 nyuma ambao wataamua ni mgombea yupi kumunga mkono.

Akizungumza na maelfu ya wafuasi wake mjini Paris alisema, “katika kipindi cha mwaka mmoja tumebadili kabisa taswira ya siasa za Ufaransa.”

Emmanuel Macron,akipiga kura yake pamoja na mkewe Brigitte, mjini Le Touquet, kaskazini ya Ufaransa. April 23, 2017.

Alisema anataka kua rais wa wafaransa wote na kutoa wito kwa wapiga kura kujitokeza kuzuia ushindi wa mrengo wa kulia wenye itikadi kali.

Bi. Le Pen anaepata ushindi kama alivyofanya babake miaka 15 iliyopita amesema “wakati umefika kuwakomboa wafaransa”.

Tayari wagombea wote wa vyama vikuu wametangaza watamunga mkono Macron katika juhudi za kumzuia Le Pen kupata ushindi.

Mshindi anatakiwa kupata zaidi ya nusu za kura zote wakati wa duru ya pili ya uchaguzi, hapo Mei 7.