Andrew Puzder, mfanyabiashara wa migahawa aliyeteuliwa na rais Donald trump kuwa waziri wa kazi, aliondoa jina lake Jumatanmo jioni, siku moja tu kabla ya kufika mbele ya kikao cha senate, kilichokuwa kinajitayarisha kumhoji kuhusiana na uwezo wake wa kuiongoza wizara hiyo.
Puzder ndiye mtu wa kwanza kwa wale walioteuliwa kuhudumu katika baraza la mawaziri la Trump kujiondoa, huku kukiwa na tetesi kwamba huenda asingepata uungaji mkono wa kutosha, kupelekea kuidhinishwa kwake na baraza la seneti.
Puzder, anayemiliki kampuni ya CRK, ambayo inakodisha migahawa kama vile Hardees na Carl’s Jr, amekuwa akikabiliwa na msururu wa utata, malalamiko na tuhuma kwamba huenda asiweze kutekeleza kazi hiyo kwa uadilifu.