Cameroon mabingwa wa kandanda Afrika

Cameroon mabingwa wa Kombe la Afrikia 2017

Wacameroon wamesherehekea usiku mzima ushindi wa timu yao iliyonyakua Kombe la Afrika la Mataifa AFCON siku ya Jumapiliu mjini Libreville, Gabon, baada ya kuilaza Misri mabao mawili kwa moja.

Ushindi huo unamaliza ukame wa miaka 15 wa Simba wa Cameroon na kusherehekea ushindi wao wa tano wa kulinyakua kombe hilo.

Ushindi ulipatikana kutokana na mkwaju usotajariwa wa Vinncent Aboubacar dakika mbili kabla ya kumalizika mchezo.

Misri iliuwona mlango kwanza katika nusu ya kwanza kutokana na goli la mchezaji wa Arsenal, Mohamed Elneny, na kuipatia Wamisri matumaini ya ushindi baada ya kutoshiriki katika finali hizo tangu 2010.

Wachezaji wa Misri washerehekea bao la kwanza

Lakini wachezaji wawili wa waloingia katika nusu ya pili upande wa Cameroon, Nicolas Nkoulou na Aboubara walibadilisha mambo na kuipatia timu yao ushindi walosubiri kwa muda mrefu.

Ushindi pia ulikua kwa kocha Hugo Broos, kutoka Ubelgiji aliyekabiliwa na mivutano mikali na vyombo vya habari tangu kuteuliwa mwezi Februari mwaka jana na kuahidi kubadilisha kabisa timu hiyo.

"Mimi hufanya kazi kupata matokeo mazuri, na ninafuraha kupindukia kwani tumepata ushindi wa CAN hii leo. Jambo pekee nililowaambia wachezaji na kuwaomba, kwa sababu tulifanya kazi nyingi kwa bidi mnamo miezi michachache iliyopita ni kua na subira na kuheshimiana, na nina matumaini vyombo vya habari vitafahamu sasa. Sina tatizo ikiwa mwandishi habari ana mkosoa mchezaji wangu au uwamuzi ninaoufanya, au chechote kile. Lakini ni lazima iwe kwa heshima."

Mashabiki wa Cameroon wakiwa na furaha na hamasa wanasema

Sisi ni mabingwa wa Afrika kwa mara nyingine. Tuna nyota tano sasa. Wamisri wametushina mara nyingi sana, hadi kufikia hii leo ilibidi kwenda kuwaona mababu wetu. tumeshinda tunafuraha kupindukia ni ushindi wa Afrika ya Kati.

Misri iliyokua na matumaini makubwa kuweza kiunaykua kombe hilko baada ya miaka 10 kutoshiriki katika finali ililazimika kuwatumia wachezaji wake wawili wenye ujuzi Ahmed Fathi na keeper Essam El Hadarywalocheza kwa pamoja mara saba katika finali ya Kombe hilo la Afrika.

Lakini kocha wao Hector Cuper anasema hawakuweza kufua dafu na anasikitika kwa ajili ya mashabiki wa Misri lakini aliwapongeza wapinzani wake.

"Kwanza kabisa nina wapongeza Cameroon kwa kushinda kombe hili. Wamecheza vizuri kabisa na wanastahiki kushinda. Bila shaka nina sikitika na kukasirika lakini uskitifu wangu mkubwa ni kwa watu wa Misri. Kwa hakika nilitaka wawe na furaha hii leo kwa kushinda kombe hili."

Keeper wa Cameroon akiokoa bao

Huko Cameroon kila pembe ya nchi ilikua katika furaha na kusherehekea kutokana na ushindi huo ambao hakuna aliyetarajia timu yao kuwasili katika finali hiyo ukilinganisha na timu za Ghana Senegal na Ivory Coast. Lakini wahenga wanakuambia hadi kipengere cha mwisho hakuna anaejua nani anaweza kushinda katika kandanda . Basi hongera kwa Simba wa Cameroon.