Mahakama yaamuru uongozi wa Trump na Jimbo la Washington kupeleka hoja zaidi

Rais Donald Trump

Mahakama ya Rufaa huko San Francisco imeutaka uongozi wa Trump na Jimbo la Washington mapema Jumapili kupeleka hoja zaidi siku ya Jumatatu mchana.

Mahakama hiyo pia imetupilia mbali ombi la uongozi wa Trump ukiitaka mara moja iendeleze amri ya kiutendaji ya Rais inayokataza kwa muda wananchi wa nchi saba zenye waislamu wengi kuingia Marekani.

Kaimu Mwanasheria anayeiwakilisha serikali kuu akitoa maelezo ya Serikali Jumamosi alinang’ania kuwa amri ya rais kwa “upana zaidi inakinga dhidi ya hatua za mahakama” iwapo nani anaweza kuingia au kubakia nchini.

Wizara ya Sheria ya Marekani ilikata rufaa jioni Jumamosi—mapema sana Jumapili, nyakati za Washington--- kujibu amri ya mahakama ya jaji wa mahakama ya rufaa iliyositisha kwa muda amri ya rais Trump inayo kataza wahamiaji kutoka nchi saba zenye waislamu wengi zaidi wasiingie Marekani.

Rufaa ya Wizara ya Sheria imesema amri ya jaji "haifahamu tafsiri ya kipimo cha rais juu ya usalama wa taifa" na itakuwa na madhara kwa umma ikiendelea “kuzuia utekelezaji” wa amri ya kiutendaji ya Trump.