Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 08:01

Jaji atoa uamuzi wa muda kusitisha amri ya Trump kuhusu uhamiaji


Mwanasheria Mkuu wa jimbo la Washington, Bob Ferguson
Mwanasheria Mkuu wa jimbo la Washington, Bob Ferguson

Jaji wa Mahakama ya Rufaa katika Jimbo la Washington amezuia kwa muda nchi nzima amri iliyotolewa wiki iliyopita kukataza wahamiaji kutoka nchi saba zenye waislamu wengi kuingia Marekani.

Maafisa wa uhamiaji na ulinzi wa mipaka Marekani tangu itoke amri ya mahakama wamesema wasafiri wenye viza halali wataruhusiwa kuingia nchini.

Baadae jioni White House ilitoa tamko likisema Wizara ya Sheria “ kwa haraka” itafungua “ombi la dharura la kuzuia amri ya kusikitisha ya mahakama.” Baada ya muda mfupi, White House ikatoa tamko jingine bila ya kutaja neno “kusikitisha.”

Tamko hilo pia limetetea amri ya kiutendaji ya Rais Donald Trump kuwa ni ya kisheria na inastahiki.”

Jaji James Robert wa Seattle alitoa uamuzi Ijumaa kuwa jimbo la Washington na Minnesota wana misingi ya kisheria kupiga amri ya kiutendaji ya Rais Trump iliyotolewa wiki iliyopita.

Jimbo la Washington lilifungua kesi kupinga amri hiyo wiki hii, na Minnesota mara moja ikajiunga katika kesi hiyo. Majimbo hayo mawili yameshinda amri ya kusitisha katazo la Trump wakati mahakama ikifikiria kesi hiyo.

Mtu nje ya Mahakama ya Rufaa akiunga mkono maamuzi ya mahakama
Mtu nje ya Mahakama ya Rufaa akiunga mkono maamuzi ya mahakama

“Katiba imeshika hatamu leo,” mwanasheria mkuu wa Washington Jenerali Bob Ferguson amewaambia waandishi wa habari Ijumaa.

Amesema kuwa uamuzi wa mahakama umesitisha mara moja kile alichokiita “ubatili wa amri ya kiutendaji ya Trump na kuwa ni kinyume cha katiba.”

“Sheria ni kitu chenye nguvu,” aliongeza kusema. “Ina uwezo wa kumwajibisha mtu yeyote, akiwemo rais wa Marekani.

Wakati huo huo Jaji wa Mahakama ya Rufaa katika mji wa Detroit ametoa amri ya muda Ijumaa kuzuia uongozi wa Trump kukataza watu kusafiri.

Amri hiyo, iliyotolewa kufuatia ombi la umoja wa kupigania haki za raia kinachowaunganisha waarabu na wamarekani, inathibitisha kuwa katazo la kusafiri haliwahusishi wenye hati halali za ukazi wakiwemo wale wenye “green card.”

Amri ya siku 90 inayowakataza raia wa nchi saba inaungwa mkono na nusu ya wamarekani wote, kwa mujibu wa tafiti nyingi, na linakwenda sambamba na ahadi alizotoa Trump wakati wa kampeni za uchaguzi.

Wakati amri hiyo haipendezi nchi za nje, Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani, John Kelly amesema kuwa amri hiyo haiwakusudii waislamu, akiongeza kuwa idara yake “inajukumu” la kuhakikisha usalama wa watu wamarekani, nchi yetu, maadili yetu.”

XS
SM
MD
LG