Katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya uwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia, Jumatatu mpinzani wake Moussa Mahamat kutoka Chad, alimshinda Bi Mohamed kwa kura 38 kwenye duru ya saba ya uchaguzi huo.
Katika uchaguzi huo Burundi, Uganda na Djibouti zilimpa kura zao Mahamat na Tanzania kuzuilia kura yake.
Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa Bi Mohamed ameonyesha kuudhiwa na msimamo wa nchi hizo na kusema kuwa Kenya itabidi ifanye tathmini upya juu ya uhusiano wake na nchi jirani za Afrika Mashariki.
Nchi ya Kenya ilikuwa imefanya kampeni kubwa kiasi kwamba Rais Uhuru Kenyatta alituma wajumbe kwenye mataifa 53 kuzishawishi zimpigie kura mwanadiplomasia huyo wa Kenya.
Hatimaye waziri huyo wa Kenya alishika nafasi ya pili baada ya kupata kura 25 dhidi ya Mahamat aliyepata 28.
Mchambuzi wa maswala ya kisiasa katika eneo la Afrika Mashariki Maur Mwanamaka, amezungumza na Sauti ya Amerika na hivi ndivyo alivyosema:
Your browser doesn’t support HTML5
Imetayarishwa na Mwandishi wetu Harrison Kamau, Washington DC