Wasifu wa Musa Faki Mahamat, mwenyekiti mpya wa tume ya AU

Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika.

Mousa Faki Mahamat alizaliwa tarehe 21 mwezi Juni, mwaka wa 1961 nchini Chad, na amekuwa waziri wa mambo ya nje wa Chad tangu mwaka wa 2009, akiwa mwanachama wa chama kinachotawala cha Patriotic Salvation Movement.

Kabla ya hapo, alikuwa waziri mkuu wa kumi na moja Chad, kati ya mwaka wa 2009 na 2010.

Mahamat ameshikilia nyadhifa mbali mbali katika serikali inayoongozwa na rais Idris Derby na ni mmoja wa wandani wa muda mrefu wa rais huyo.

Mwansiasa huyo si mpya katika maswaloa ya umoja wa Afrika, kwani amewahi kuhudumu kama mwenyekiti wa Almashauri ya Umoja huo, kuhusu uchumi, maswala ya jamii na utamaduni kati yam waka wa 2007 na 2008.

Mahamat ameoa na wamejaliwa na watoto watano.

Alipata kura 38 kwenye duru ya saba ya uchaguzi wa leo, na hivyo basi kutangazwa mshindi baada ya kupata angalau theluthi mbili ya kura zoite zilizopigwa.