Obama kuchukua hatua dhidi ya serikali itakayoingilia uchaguzi wa Marekani

Rais Barack Obama akitoa maelezo kwenye mkutano wa My Brother’s Keeper Summit, White House jijini Washington, Disemba14, 2016

Rais wa Marekani Barack Obama amesema serikali itachukua hatua dhidi ya Rashia au serikali nyingine yoyote ambayo inajaribu kuingilia uchanguzi wa Marekani.

“Nafikiri hakuna shaka kwamba pale serikali ya kigeni inapojaribu kuharibu uaminifu na maadili thaniti ya uchaguzi wetu…tunalazimika kuchukua hatua. Na tutakabiliana na hilo, “rais aliiambia redio ya NPR katika mahojiano ambayo yatatangazwa Ijumaa asubuhi.

“Baadhi ya hizo hatua ziko wazi na zitaelezewa, lakini baadhi hazitaelezwa,” alisema Rais Obama.

Idara ya ujasusi ya Marekani, CIA, iliamua kwamba wadukuzi wa Rashia walishambulia kompyuta za Chama cha Demokrat ili kuchapisha barua pepe za siri, zenye kudhalilisha kampeni ya urais ya Hillary Clinton ikiwa ni ishara tosha ya msaada waliotoa kwa Donald Trump wa Republican kushinda uchaguzi mwezi uliopita.

Maafisa: Putin alijua

Mafisa wa juu wa White House wanasema vitimbi hivi visingeweza kutokea bila ya Rais Vladimir Putin kuhusika au kuwa na taarifa. Moscow imekiita kisa hiki ni “dhihaka ya kipuuzi.”

Obama ameiambia NPR kuwa bado kuna “mlolongo wa tathmini” unaoendelea katika idara za ujasusi za Marekani, na anasubiri ripoti ya mwisho juu ya nani hasa alihusika na ni kwa sababu gani.

“Lakini hilo kwa namna yoyote ile halidhoofishi hoja ya msingi kwamba kila mtu wakati wa uchaguzi alikuwa na maoni sahihi kwamba udukuzi wa Rashia kwa bhakika ulisababisha matataizo makubwa zaidi kwa kampeni ya Clinton kuliko kile walichofanya katika kampeni ya Trump,” Obama amesema.

Trump, hata hivyo, ameuliza katika ujumbe wake wa Twitter, “iwapo Rashia, au taasisi nyingine ilikuwa ikifanya hujuma hizo, kwa nini White House ilisubiri muda mrefu kuchukua hatua? Kwa nini walilalamika tu pale Hillary aliposhindwa?

Obama alikata kusema iwapo anafikiria kuwa hujuma ya mtandao iliyofanywa na Rashia ilimsababisha Hillary Clinton kushindwa katika uchaguzi. Alisema kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kubadilisha mwelekeo wa kura za urais, lakini hakukuwa na shaka kwamba ilikuwa na athari.

Pia hakusema iwapo anaamini kampeni ya Trump ilihusika kwa namna fulani katika hujuma hiyo mbali na kuzitumia hizo email zilizovuja kwa maslahi ya kisiasa.

Obama alisema ameshtutushwa na kunang’ania kwa Trump kwamba Rashia haikuhusika na kuhujumu kompyuta za Chama cha Demoktrati, na kwa msimamo wa rais mteule kuisaidia Rassia.

“”Kumekuwa na idadi kubwa ya wanachama wa republikani wanaonang’ania kunikosoa kwa kutokuwa na msimamo mkali juu ya Rashia,” alisema. “Wengine kati yao wakati wa Kampeni walimpitisha Donald Trump… huku kukosa msimamo inaonyesha kwamba msimamo wao hasa juu ya Rassia katika siku yoyote inategemea wana utashi gani wa kisiasa.

Ben Rhodes, mshauri wa juu was mambo ya nje wa Obama, ameiambia kituo cha televisheni cha MSNBC, “Kile ambacho tunafahamu kuhusu operesheni za Rashia na jinsi gani Putin anavyodhibiti serikali hiyo, na unapozungumzia shambulizi kuu la mtandao, basi hapo tunazungumzia kuhusika kwa serikali katika ngazi ya juu. Na hatimaye, Vladimir Putin ndio mhusika mkuu kwa vitendo vyote vya serikali ya Rashia.

Msemaji wa White House Josh Earnest akizungumza ikulu Washington, Dec. 8, 2016.

Msemaji wa Ikulu ya White House Josh Earnest, akizungumza na waandishi, alielezea tathmini ya jumuiya ya kintelijensia ya Marekani iliyotoka Oktoba kuwa “ni maafisa wa juu wa Rashia pekee wangeweza kuidhinisha hujuma hii.”

Alisema kurejeshwa kwa hujuma hii kwa maafisa hawa sio kwa kubuni. “Hili ni jambo la wazi,” alisema.

Mmoja wa wasaidizi wa Trump, Kellyanne Conway, katika mahojiano alimshukia Earnest kwa kusema Jumatano kuwa inawezekana Trump alikuwa anajua hujuma ya Rashia wakati kampeni kwenye mchakato wa Uchaguzi wa Urais wa Marekeni unaendelea na kuwa “kuingilia kati kwao kumeleta athari mbaya” juu ya kampeni ya Clinton.

Kellyanne Conway, mshauri wa juu katika kipindi cha mpito cha Donald Trumo

“Hayo ni maajabu," alisema Conway ameiambia shirika la televisheni ya Fox News."Nadhani anajaribu kujiandaa kuwa mchambuzi wa kisiasa baada ya kumaliza ungwe yake Ikulu ya Marekani. Pia inashitua sana kusikia kutoka kwa msemaji wa White House. Kwa sababu kimsingi- kubwa alilosema ni kuwa rais-mteule alikuwa na taarifa juu ya hujuma hii, na pengine alichochea jambo hili. Hii ni hali ya kusikitisha kwa kutokuwa kwake makini na sijui kama bosi wake Rais Obama anakubaliana nae.”

Siku ya Alhamisi, Earnest pia alirudia tena kuhusu tamko lake hilo kwamba Trump sio tu alijua hujuma hiyo ya Rashia wakati wa kampeni lakini pia aliwahamasisha.