Fidel Castro afariki akiwa na umri wa miaka 90

Fidel Castro akiwa amekaa na kumshika mkono kakake, rais wa Cuba Raul Castro, kulia, na naibu katibu wa pili wa chama tawala.Jose Ramon Machado Ventura,

Kiongozi wa muda mrefu wa Cuba Fidel Castro afariki baada ya kuugua kwa muda mrefu Ijuma usiku kufuatana na televisheni ya Cuba.

Taarifa haikutoa maelezo zaidi.

Fidel Castro kiongozi wa chama cha kikomunisti cha Cuba aliongioza taifa hilo lkwa karibu nusu karne kabla ya kumkabidhi mamlaka kakale Raul 2008.

Castro alichukua madaraka 1959, akiwa na umri wa miaka 32 akiongoza kundi dogo lwa wanamapinduzi kuiangusha serikali ya kimabavu ya Fulgencio Batista, na kuahidi kuleta mabadiliko ya kidfemokrasia na kumaliza ukandamizaji.

FILE - Waziri mkuu wa Cuba Fidel Castro aliyepindua serikali ya Fulgencio Batista Jan. 1, 1959.

Haikuchukua muda ahadi ilivunjwa na mwanamapinduzi Castro, akanzisha utawala wa kikomunisti na kuliongoza taifa hilo kwa miaka 47 hadi pale ufonjwa wa matumbo kumlazimisha kuacha madaraka na kumkabidhi mdogo wake Raul.

Mnamo muda wote wa utawala wake hasimu mkuu alikua Marekani aliyeiwekea nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi ambavyo Castro alibahatika kushuhudia vikiondoshwa mwaka 2015 na Rais Barack Obama.