Peres alipatwa na ugonjwa wa kiharusi wiki mbili zilizopita na amefariki Jumatano katika hospitali ya Tel HaShomer.
Aliyekuwa Rais wa zamani na waziri mkuu wa Israel Shimon Pres amefariki akiwa na umri wa miaka 93.
Peres alipatwa na ugonjwa wa kiharusi wiki mbili zilizopita na amefariki Jumatano katika hospitali ya Tel HaShomer.
Wakati wa uhai wake aliweza kushika madaraka mengi katika ngazi za kisiasa , ikiwemo kuwa waziri mkuu mara mbili , rais , waziri wa ulinzi na waziri wa mambo nje .
Alikuwa ni kingozi aliyehudumu kwa muda mrefu kwenye bunge katika historia ya Israel akishikilia kiti kwa miaka 48.
Peres alizaliwa huko Belarus mwaka 1923 na kuhamia Israel alipokuwa na umri wa miaka 11 wakati taifa la Jewes likitawaliwa na Uingereza.