Rudisha atetea medali yake ya Olimpiki

David Lekuta Rudisha (kulia), wa Kenya

Bingwa wa mbio za mita 800 duniani David Rudisha ametetea medali yake ya dhahabu katika mbio hizo kwenye mashindano ya Olimpiki kwa kushinda fainali Jumatatu usiku Rio de Janeiro.

Kwa ushindi huo Rudisha ametetea medali yake ya dhahabu aliyoshinda katika michezo ya Olimpiki ya London 2012. Kwa ushindi huo pia Rudisha ameipatia Kenya medali ya pili a dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya Rio.

Jemimah Sumgong

Jumapili mwanadada Jemima Sumgoong alishinda medali ya dhahabu katika mbio ndefu za marathon. Kenya pia imeshinda medali nyingine tatu za fedha katika Olimpiki za Rio mpaka sasa.

Ikiwa na jumla ya medali tano Kenya inashikilia nafasi ya pili kwa nchi Afrika baada ya Afrika Kusini ambayo mpaka sasa ina jumla ya medali sita, moja ya dhahabu, nne za fedha na moja ya shaba.

Katika fainali za mita 800 Ferguson Rotich naye pia wa Kenya alishindwa kupata medali baada ya kupitwa katika dakika za mwisho na washindani wengine.