Katibu mkuu kiongozi mpya wa Tanzania aapishwa

Rais wa Tanzania John Magufuli

Rais John Magufuli alitangaza kumpangia kazi nyingine balozi Ombeni sefue aliyemteua tena kuwa katibu mkuu kiongozi desemba 30 mwaka jana baada ya yeye kuingia madarakani.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amemwapisha katibu mkuu kiongozi mpya John Kijazi huku kuondolewa kwa aliyekuwa katibu mkuu kiongozi ombeni sefue kukizua gumzo nchini humo

Rais John Magufuli alitangaza kumpangia kazi nyingine balozi Ombeni sefue aliyemteua tena kuwa katibu mkuu kiongozi desemba 30 mwaka jana baada ya yeye kuingia madarakani

wengi wamehoji kuhusu mabadiliko hayo kwa kura arais hakusema sababu za kumuondoa Sefue.

Your browser doesn’t support HTML5

Mabadiliko ya uongozi Tanzania

Katibu mkuu kiongozi mpya John Kijazi kabla ya kukabidhiwa wadhifa huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India , Kijazi pia aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi.

Miongoni mwa baadhi ya watu waliohojiwa na VOA wameutathmini uongozi wa Rais Magufuli kama usio na upendeleo na unaotekeleza malengo yake aliyoyatoa awali ya “ hapa kazi tu”.