Mdahalo wa wagombea Urais wafanyika Uganda.

mmoja wa wagombea urais wa upinzani nchini Uganda Patrick Amama Mbabazi .

Moja ya mada iliyosisimua ni kuhusu sekta afya ambapo wengi wa wagombea wamesema mfumo wake umeharibika

Wagombea urais nchini Uganda jana wameshiriki mdahalo wa pamoja ulioangazia maswala ya uchumi, afya, elimu, demokrasia na maendeleo katika jamii. Rais wa sasa Yoweri Museveni hata hivyo amesusia mdahalo huo.

Ni mdahalo uliochukua masaa manne unaosemekana kujaa maswali na majibu ya kuchekesha. Mdahalo huo ulihudhburiwa na wagombea urais saba ikiwemo Dr kiza besigye ambaye alieleza kukasirishwa kwake dhidi ya waandaaji wa mdahalo akisema walimdanganya na kumfanya ashiriki wakijua kwamba rais Museveni hatakuwepo.

Moja ya mada iliyosisimua ni kuhusu sekta afya ambapo wengi wa wagombea wamesema mfumo wake umeharibika.

Kuhusu kilichopo kwenye mikataba ya serikali kwa upande wa mafuta hakuna mgombea aliyeonyesha kujua zaidi akiwemo Patrick Amama Mbambazi ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu wa serikali ya Museveni.

Wagombea wote wamekubali kwamba uchumi wa Uganda uko taabani, ufisadi umekithiri na fedha za serikali zinatumika vibaya.