Obama awakosoa Warepublican

Jengo la bunge la Marekani

Rais wa Marekani, Barack Obama, amekosoa kundi la maseneta 47 wa chama cha Republican ambao waliionya Iran, kwamba makubaliano yeyote ya nyuklia itakayofikia na Rais Obama yataweza kudumu hadi atakapoondoka madarakani mapema 2017 .

Bwana Obama, aliwaambia wanahabari White House, kwamba vitendo vya Warepublican, ni vya ajabu kwasababu wanaonekana wanajiweka sambaba na wale wenye siasa kali huko Iran.

Amesema huo si muungano wa kawaida.

Naye waziri wa mambo ya nje wa Iran, Javad Zarif, pia alikosoa barua ya Warepublican, kwa kusema hawana haki kisheria na ni njama za kipropaganda.

Amesema kama uongozi mpya wa Marekani utabatilisha makubaliano na Iran, itakuwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.