Mkuu wa mawaziri 19 wa fedha wa umoja wa Ulaya, ametoa mwito kwa Ugiriki, kutopoteza muda na kuharakisha mazungumzo ya kutekeleza program mpya ili kuweza kupata mikopo ya kimataifa ya uokozi.
Mwenyekiti wa kundi hilo Jeroen Dijsselbloen, amesema machache yamefanyika toka mkutano wa mwisho wa kundi hilo kwa upande wa mazungumzo na utekelezwaji wa mageuzi ya uchumi.
Amesema hawapaswi kupoteza muda mwingi, kwa kuwa muda ulioongezwa ni miezi minne tu na muda unakwenda.
Wiki iliyopita waziri wa fedha wa Ugiriki, Yanis Varouvakis, aliorodhesha mageuzi katika barua ambayo iliyotoa takwimu kidogo.
Bwana Dijsselbloem, aliasema mapendekezo yalikuwa bado hayajakamilika.
Athens ilipewa miezi mine zaidi ya kurudisha fedha za uwokozi kutoka umoja wa ulaya ifikapo mwishoni mwa mwezi June.