Uchunguzi wa maoni ulofanywa na kituo cha televisheni cha CNN mara tu baada ya mdahalo, unaonesha kwamba asili mia 67 ya wapiga kura walohojiwa wanasema Romney alimshinda Obama kwenye mdahalo huo. Huku asili mia 26 wakisema Obama alifanya vizuri.
Wanasiasa hao wawili kwa sehemu kubwa walizungumzia uchumi, na namna ya kubuni nafasi za ajira na mipango yao ya kodi na afya.
Mitt Romney anasema ni lazima kutafuta njia nyingine ya kubuni ajira akisema mipango yake ni pamoja na kuongeza uzalishaji nishati, kupanua biashara ya kimataifa, kubuni nafasi zaidi ya mafunzo ya kazi na kuleta uwiyanio katika bajeti.
“Ndio tunaweza kuleta mabadiliko, na si kutumia njia tuliyo nayo sasa ambayo rais anaeleza ni kuongeza kodi kwa matajiri na kupunguza wa watu wa tabaka la chini. Mimi sitompunguzia mtu kodi kwa wakati huu mgumu wa uchumi. Mimi nina nukta tano ya mageuzi, kupanua uchimbaji mafuta na hivyo kupatikana nafasi milioni 4 za ajira, kupanua masoko ya Amerika Kusini kwa biodhaa ya Marekani, kuadhibu China wanapodanganya, wamarekani wapate ujuzi unaohitajika kwa kazi na kuhamasisha biashara ndogo ndogo.” alisema Romney.
Kwa upande wake Obama anasema anakubaliana na Romney kuimarisha uzalishaji nishati lakini anasema kwa kuangalia namna ya kutumia teknolojia ya kisasa ya nishati mbadala ya juwa na upepo na kurudisha nafasi za kazi zilizosafirishwa nje ya nchi.
“Suala hii leo si tulikuwa wapi, bali ni tunakwenda wapi, Romney anataka kuwapunguzia matajiri kodi na kupunguza usimamizi katika biashara kubwa. Mimi ninataka kutumia pesa kwa ajili ya elimu na mafunzo ya kazi, nishati mbadala na kubadili kanuni za kodi. Na kutumia fedha zinazopatikana kwa kumaliza vita viwili na kutumia kukarabati Marekani,” alisema rais Obama.
Suala jingine waliozungumza kwa urefu na muhimu ni mpango wa mageuzi ya huduma ya afya maarufu kwa jina la ‘Obamacare’. Romney anapinga mpanmgo huo akisema haijabidi kwa serikali kuu kuamrisha watu na madaktari juu ya kile kilicho bora kwa afya yao.
Anasema inabidi kuachia mashoko na biashara kuendesha huduma za afya.
Obama anapinga wazo hilo akisema huo ni mpango Romney aliupitisha akiwa Gavana wa Massachusetts.
“Ukifutilia mabli mpango huo wa ‘Obamacare’ - jina ambalo nimeanza kupenda - mara moja wazee watajikuta wanalipa dola mia 600 zaidi kwa ajili ya dawa na matibabu na gharama nyenginezo. Na watu watakaofaidika kutokana na kufutiliwa mpango huo ni makampuni ya bima.” alisema Obama.
Mbali na hayo Obama na Romney walizungumzia maoni yao juu ya jukumu la serikali kuu. Obama akisema kuna tofauti kati yao yeye akiamini jukumu la kwanza la serikali ni kuwalinda wananchi, pili kuwapatia elimu, hivyo anataka kuajiri walimu zaidi hasa wa sayansi na teknolojia ili Marekani iweze kuongeza tenakatika fani hizo.
Romney anasema inabidi watu binafsi wawajibike na kuacha majimbo kuongoza katika elimu.
Wachambuzi wamegawika juu ya nani aliyeshinda kinyume na wapiga kura waloamua kwamba Romney anmeshinda.
Mhadhir wa chuo kikuu cha Florida Charles Bwenge anasema kila mmoja kati ya wagombea hao wawili walichukua tahadhari na hakuna aliyepata ushindi, ingawa anasema Obama alikuwa na fursa ya kumtwanga ngumi ya kumangusha chini.
Mdahalo huu ulosubiriwa kwa hamu ulifanyika mjini Denver Colorado , siku 34 kabla ya uchaguzi mkuu.
Joseph Lowndes profesa wa sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Oregon anasema mdahalo wa kanza daima ni muhimu na anahisi wagombea wote wanmefanya vyema, na hata ikiwa wapiga kura wanahisi Romney amefanya vyema zaidi lakini hadhani amepata natija za kutosha kuweZa kubadili matokeo ya maoni jumla ya wananchi.

Your browser doesn’t support HTML5