Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 01:36

Zuma azungumza na Mugabe


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (kushoto) na mkewe Grace
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (kushoto) na mkewe Grace

Rais wa Africa Kusini amesema kiongozi aliyekuwa kwenye madaraka kwa muda mrefu Zimbabwe Robert Mugabe “amezuiliwa nyumbani kwake” katika kile kinachoonekana kuwa ni juhudi za kijeshi zinazoendelea kumuondoa katika madaraka baada ya miaka 37 ya utawala wake.

Rais Jacob Zuma, ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi zilizoko Kusini mwa Afrika (SADC) amesema katika tamko lake amezungumza mapema Jumatano na Rais Robert Mugabe “ambaye amegusia kuwa amezuiliwa nyumbani kwake, lakini amesema hana tatizo lolote. Afrika Kusini pia inafanya mawasiliano na Jeshi la Ulinzi la Zimbabwe.”

Yale yanayoendelea kutokea ni kutokana na vitendo vya Mugabe ambavyo vimempotezea umaarufu ambapo alimfukuza makamu wake, Emmerson Mnangagwa, na kusema kuwa ana mpango wa kumweka mkewe madarakani baada ya kumng’oa makamu wa rais.

Matenki ya kivita yaliingia katika mji mkuu wa Harare Jumanne, siku moja baada ya mkuu wa majeshi ya Zimbabwe, Jenerali Constantino Chiwenga, alipoonya kuwa “ataingilia kati” iwapo Mugabe hatoacha kuwaondoa wafuasi wa Mnangagwa wa chama cha ZANU-PF. Dazeni ya watu wamekamatwa tangia makamu wa rais alipofukuzwa kutoka katika wadhifa wake Novemba 5. Chama tawala cha Zimbabwe kimemtuhumu Chiwenga kwa kosa la uhaini baada ya kutoa tamko lake.Wanajeshi walikiteka kituo cha televisheni mapema Jumatano.

“Tunapenda kuliweka suala hili wazi kabisa kuwa haya siyo mapinduzi ya kijeshi kwa ajili ya kuchukua madaraka,” msemaji wa jeshi Meja Jenerali SB Moyo amesema.

Kile ambacho Jeshi la Ulinzi la Zimbabwe linafanya ni kuleta utulivu wa kisiasa , kijamii na kiuchumi ndani ya nchi, na kama hatua hii haijachukuliwa inaweza kupelekea machafuko ya kivita.

Chama tawala cha Zimbabwe kimesema katika mitandao ya kijamii kuwa Mnangagwa atarudi madarakani. Lakini mpaka sasa hajulikani aliko, sema kuna minongono kuwa yuko Afrika Kusini.

XS
SM
MD
LG