Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 20:10

Zimbabwe yazindua mchakato wa fidia ya mauaji ya 1980


Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa
Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, Jumapili amezindua mchakato uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu wa maridhiano kutokana na mauaji ya miaka ya 1980 yaliyofanywa na wanajeshi wa serikali ambayo yaligharimu maelfu ya maisha ya watu. 

Walionusurika watahojiwa katika mfululizo wa vikao vinavyofungua njia ya uwezekano wa kulipwa fidia, kwa nia ya kusuluhisha malalamiko na mivutano ya muda mrefu.

β€œLeo ni wakati muhimu katika historia yetu. Hii ni siku ambayo tunadhihirisha kama nchi tunaweza kutatua mizozo yetu kama Wazimbabwe, bila kujali ugumu au ukubwa wake,” Rais Mnangagwa amesema katika taifa hilo la pili kwa ukubwa kusini mwa Afrika, katika mji wa Bulawayo.

Amesema mpango huo ni ishara na nia ya pamoja ya kuondoa migawanyiko ambayo imetenganisha Wazimbabwe kwa muda mrefu.

Mauaji hayo yanayoitwa Gukurahundi yalifanyika miaka michache baada ya Zimbabwe kupata uhuru kutoka Uingereza, huku kiongozi wa zamani Robert Mugabe akisisitiza mamlaka yake.

Kuanzia 1983, Mugabe alituma kikosi cha wasomi kilichopata mafunzo Korea Kaskazini kukabiliana na uasi katika eneo la Matabeleland magharibi mwa Bulawayo, kitovu cha watu wa kabila la Wandebele walio wachache.

Waliua takriban watu 20,000 kwa miaka kadhaa, kwa mujibu wa Tume ya Katoliki ya Haki na Amani ya Zimbabwe, idadi inayokubaliwa na Amnesty International.

Wakosoaji wanasema ililenga wapinzani wa Mugabe, waliomuunga mkono kiongozi mwenza wa mapinduzi Joshua Nkomo, ambao wengi walikuwa kutoka kabila la Wandebele.

Forum

​
XS
SM
MD
LG