Rais wa Marekani, Barack Obama, atakuwepo mjini Orlando, Florida leo kufanya kile “White House” ilichokiita “wajibu wake wa kufariji na kutoa pole kwa jumuiya hiyo inayopitia kipindi kigumu."
Ziara yake inatokana na mauaji ya Jumapili katika klabu ya wapenzi wa jinsia moja katika mji huo ya watu 49 na kujeruhiwa watu 53 wengine.
Rais Obama atakutana na familia za walioathirika, na wale walionusurika pamoja na polisi, vikosi vya dharura na uokoaji, wauguzi, madaktari na wakiwemo wale bingwa wa upasuaji waliosaidia katika kuwahudumia wale wote waliopigwa risasi.
Wakati huo huo kamati ya mambo ya ndani ya baraza la Seneti la Marekani limetoa wito kwa ukurasa wa tovuti ya Facebook kutoa taarifa zote zinazowezekana na akaunti yoyote inayohusiana na aliyefanya shambulizi hilo Omar Mateen.