Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 11:22

Ziara ya Obama Kenya Yaimarisha Usalama


Picha ya rais Barack Obama wa Marekani.
Picha ya rais Barack Obama wa Marekani.

Tangu hapo serikali iliweka kamera zaidi na idara za usalama zitategemea zaidi kamera za CCTV kama sehemu ya usalama wakati wa ziara ya rais Barack Obama. Mkurugenzi wa Barabara katika county ya Nairobi Mohamed Abdullahi amesema matatizo ya awali yametatuliwa.

Vikosi vya usalama vya Kenya vitategemea zaidi kutumia mfumo wa kamera za usalama za kudhibitiwa maeneo maalum maarufu kwa jina la CCTV kote jijini Nairobi ili kuhakikisha usalama wakati wa ziara ya rais Barack Obama mwezi huu. Lakini kama anavyoripoti mwandishi wetu mohammed yusuf , kwamba katika siku za nyuma mfumo huo wa kamera haukufanya kazi kama ilivyotekemewa.

Rais obama na mkewe Michelle
Rais obama na mkewe Michelle

Mfumo huo wa kamera haukufanya kazi katika eneo hili la tukio la uhalifu ambako mbunge George Muchai na mlinzi na dereva wake waliuliwa kwa majira ya jioni February saba .

Shambulizi lilitokea katikati mwa mji, sio mbali na majengo ya serikali yanayolindwa na maafisa wa usalama na kamera hizo za usalama za CCTV.

Kamera hizo mpya zilizowekwa zilitarajiwa kuwasaidia polisi kuwatambua wauwaji.

Na kwa hakika usiku huo tukio lilirikodiwa na kamera hizi zilizowekwa juu ya jengo hili lenye ghorofa 24.

Lakini picha ya video ambayo VOA iliweza kuipata kwa siri kuhusiana na tukio hilo haioneshi vizuri kinachotokea au kuwatambua .

Alis Lentoimaga makamu mwenyekiti wa kamati ya usalama ya bunge , amesema CCTV zimeshindwa kuwagundua wauwaji.

Anasema uchunguzi ulifanyika kwa kina, kulikuwa na vyombo vingine vilivyotumiwa, hasa simu , kutokana na simu baadhi ya watu hao walikamatwa kwa sababu hiyo.. na siyo kwa sababu ya CCTV kwa sababu CCTV haifanyi kazi kwa ukamilifu bado.’

Tangu hapo serikali iliweka kamera zaidi na idara za usalama zitategemea zaidi kamera za CCTV kama sehemu ya usalama wakati wa ziara ya rais Barack Obama. Mkurugenzi wa Barabara katika county ya Nairobi Mohamed Abdullahi amesema matatizo ya awali yametatuliwa.

Anasema tuna taraji kuanzia barabarani hadi kwenye chumba cha udhibiti hakuna kilichohujumiwa hasa wakati unapotegemea miundombinu kama hiyo inayohusiana na mawasiliano.

Kamera hizo zimeigharimu serikali ya county takriban dola milioni 4.4 matumizi yanayoungwa mkono na polisi katika kupambana na uhalifu na kupunguza msururu mrefu wa magari.

kamera tunazo tayarisha ili kutumia njiani zitakuwa nzuri hasa katika utendaji kazi. Hatutaki kwa wakati wowote ule raia wa kenya kuhisi wamepunjwa.

Lakini wakenya wengi wanasema bado wanasubiri faida na mfumo huo kwa jiji lao..

XS
SM
MD
LG