Kiongozi huyo wa Ukraine amesema kwamba utawala wake unaamini kwamba utafanikiwa, akiongezea kwamba hajui itachukua muda gani kuanza mashambulizi hayo, lakini wapo tayari.
Amesema kwamba angependelea kuwa na silaha za kutosha kutoka nchi za magharibi.
Zelenzkyy vile vile amesema kwamba hana uhakika na mtokeo ya uchaguzi mkuu wa Marekni wa mwaka ujao 2024, kwa sababu huenda serikali isiyokuwa na nia ya kusaidia Ukraine, ikashinda uchaguzi huo.
Kiongozi huyo vile vile amesema kwamba hatua ya Ukraine kujiunga na muungano wa NATO ni hatua nzuri kabisa ya kiusalama, lakini akakiri kwamba haitawezekana hadi vita hivyo vitakapomalizika.
Alikuwa akizungumza mjini Kyiv akiwa na rais wa Estonia Alar Karis.
Forum