Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 21:56

Zelenskyy ataka ruhusa ya kushambulia Russia


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy kwa mara nyingine Jumapili ametoa wito kwa washirika wa Magharibi kuruhusu Kyiv kushambulia maeneo ya kijeshi ndani ya Russia, hasa kambi za anga, baada ya shambulizi kubwa la Kharkiv.

“Suluhu ya kimfumo pekee ndiyo inayowezesha kupinga ugaidi huu, na suluhu ya muda mrefu ya kuharibu anga za jeshi la Russia, mahali ilipo,” Zelenskyy amesema katika hotuba yake ya kila siku.

Hapo awali, bomu la Russia, lilishambulia jengo la makazi mjini Kharkiv, shambulizi la karibuni zaidi kati ya mfululizo wa mashambulio katika mji huo wa kaskazini mashariki, na kuanzisha moto ambao kikosi cha zimamoto kiliuzima.

Waokoaji walitoa maiti ya mwanamke mzee kutoka kwenye vifusi, Meya wa Kharkiv Igor Terekhov, amesema kwenye Telegram, na kuongeza kuwa watu 42 wamejeruhiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG