Katika hotuba yake ya kila usiku kwa wanainchi wa Ukraine kwa njia ya video, Zelensky aliyeonekana kuwa mwenye hasira amesema nchi za magharibi zilikosea mwaka jana kwa kuchelewesha vikwazo na uvamizi ulifuata.
“Vita kamili vimeanza. Sasa kuna vidokezo vingi na onyo zinazodaiwa kuwa vikwazo zaidi, kama vile marufuku ya uuzaji wa mafuta ya Russia barani Ulaya, itawekwa ikiwa Russia itatumia silaha za kemikali,” Zelensky amesema, akiweka mara kwa mara mikono yake juu ya meza.
Uvamizi wa Russia huko Ukraine ambao umedumu zaidi ya mwezi mmoja, mzozo mkubwa wa Ulaya tangu vita vya pili vya dunia, umepelekea zaidi ya Waukraine milioni 3.8 kukimbilia nchi jirani, huku ukiua maelfu ya watu na kujeruhi maelfu wengine, na kuitenga Russia kiuchumi.
Zelensky amesema vikwazo vinapaswa kuwa “vyenye ufanisi” na “vikali” kutokana na hatua za Russia kufikia sasa.