Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:03

Zanzibar yaadhimisha miaka 48 ya Mapinduzi


Rais wa Zanzibar, Dk Ali M. Shein na Makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif
Rais wa Zanzibar, Dk Ali M. Shein na Makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif

Sherehe za maadhimisho zilizoongozwa na Rais wa Zanzibar Dk. Mohamed Shein.

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein Alhamisi amewaongoza mamia ya wananchi wa Zanzibar katika maadhimisho ya miaka 48 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Kilele cha maadhimisho hayo kilifanyika katika uwanja wa Amani ambako kulikuwa na maandamano ya wananchi kutoka mikoa mitano ya Zanzibar yaliyopokelewa na Dk. Shein pamoja na kukagua vikosi vya ulinzi na usalama.

Viongozi mbalimbali walihudhuria maadhimisho hayo akiwemo Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na wawakilishi mbalimbali kutoka nje ya nchi na wanadiplomasia.

Kabla ya kilele chake maadhimisho hayo yalizinduliwa Januari 2 mwaka huu kwa miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile sekta za uvuvi, mawasiliano , ujenzi na majengo ya Serikali pamoja uwekaji wa mawe ya msingi katika shule za sekondari huko Zanzibar.

XS
SM
MD
LG