Takriban watu milioni 1.25 walikufa kutokana na Kifua Kikuu mwaka jana, ripoti mpya imeongeza, na kwamba huenda ugonjwa huo umerejea kwenye nafasi ya juu ya vifo na maambukizi, baada ya kupitwa na Covid-19 wakati wa janga. Idadi hiyo ni karibu mara mbili ya watu waliouwawa na HIV na Ukimwi 2023.
WHO limesema kuwa Kifua Kikuu kimeendelea kuathiri zaidi watu kutoka Kusini Mashariki mwa Asia, Africa na Magharibi mwa Pacific. India, Indonesia, China, Ufilipino na Pakistan zimerekodi zaidi ya nusu ya kesi za mambukizi kote duniani. Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa inasikitisha kuona kuwa Kifua Kikuu bado kinaambukiza na kuuwa watu wakati tukiwa na vifaa vya kutambua, kuzuia na kutibu.
Kifua Kikuu husababishwa na bacteria kupitia kwenye hewa na mara nyingi huambukiza mapafu. Inakadiriwa kuwa takriban robo ya watu duniani wana Kifua Kikuu lakini ni asilimia 5 hadi 10 pekee ambao huonyesha dalili za maambukizi.
Forum