Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 21:21

Zaidi ya watu milioni 13 wahitaji misaada ya dharura Ethiopia


Malori ya kupeleka misaada kuelekea mkoa wa Tigray, kwenye picha maktaba. Juni 09,2022
Malori ya kupeleka misaada kuelekea mkoa wa Tigray, kwenye picha maktaba. Juni 09,2022

Shirika la Afya Duniani linasema watu milioni 13.1 katika baadhi ya maeneo nchini Ethioia wanahitaji msaada wa kibinadamu na huduma za afya.

Miongoni mwa watu hao, milioni 5.2 wapo katika mkoa uliokumbwa na mzozo wa Tigray. Tangu mzozo ulipoanza kati ya serikali ln vikosi vya TPLF karibu miaka miwili iliyopita, misaada ya kibinadamu haifiki Tigray.

Sitisho la mapigano la miezi 5 lilivunjika miezi miwili iliyopita na hivyo kukatiza misaada ya kibinadamu kwa njia ya ndege au barabara. Ilham Abdelhai Nour ambaye anaongoza timu ya kudhibiti matukio pamoja operesheni za dharura kwenye WHO amesema kwamba asilimia 89 ya wakazi wa Tigray hawana usalama wa chakula huku asilimia 29 ya watoto wakikabiliwa na utapiamlo.

Ameongeza kusema kwamba asilimia 55 ya wanawake wajawazito pamoja na wanaonyoshesha wanakabiliwa na utapiamlo, wakiwa kwenye hatari ya kupata maradhi au hata kufa. Mratibu wa dharura za kifya wa Altaf Musani amesema kwamba ni asilimia 9 pekee ya vituo vya afya ndani ya Tigray zinazofanya kazi.

Ameongeza kusema kwamba zoezi la chanjo za kuzuia magonjwa limeshuka chini ya asilimia 10 mwaka huu, na kwa hivyo kuwaacha watoto wakiwa kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi yanayoweza kuzuiliwa . Ameongeza kusema kwamba WHO imeshindwa kufikisha huduma muhimu kama vile chanjo, petroli pamoja na dawa kwenye mkoa wa Tigray.

XS
SM
MD
LG