Mapigano hayo yalianza Jumanne kufuatia ripoti za kuuawa kwa afisa wa jeshi kutoka kikosi cha masuala ya dharura cha Sudan RSF.
Afisa huyo alikuwa anatoka jamii ya Rizeigat na anaripotiwa kuuawa na watu wasiojulikana.
Wengi waliouawa katika mapigano hayo ni wanawake na watoto
Afisa wa serikali ya mtaa wa Dafur ameliambia shirika la habari AFP kwamba watu 15 waliuawa katika mapigano kati ya kikabila kati ya Rizeigat na Fallata siku ya Jumanne na 30 waliuawa Jumatano.
Maafisa wa usalama wamepelekwa sehemu hiyo kurejesha hali ya utulivu.
Vita vya Dafur vilianza mwaka 2003 baada ya waasi wa kikabila kuanza vita dhidi ya serikali ya rais wa zamani Omar al-Bashir, iliyokuwa na idadi kubwa ya waarabu.