Afisa wa ngazi ya juu wa afya amethibitsha hayo leo Jumapili, na kupelekea mapigano hayo kuwa mabaya zaidi kuwahi kutokea katika eneo hilo katika miaka ya karibuni.
Sudan inakabiliwa na mapigano ya kijamii pamoja na mgogoro wa kisiasa.
Mapigano katika jimbo la Blue Nile, karibu na Ethiopia na Sudan Kusini, yalianza tena mapema mwezi huu, kutokana na mgogoro wa umiliki wa ardhi.
Watu kutoka kabila la Hausa, kutoka Afrika Magharibi, wanapigana na watu kutoka kabila la Berta.
Hali ya wasiwasi ilianza kuongezeka Jumatano na Alhamisi, katika mji wa Wad el-Mahi karibu na mpaka na Ethiopia.
Maafisa wamehesabu miili ya watu 220 na huenda idadi ya vifo ikaongezeka.