Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 11:06

Zaidi ya watu 1000 waandamana kupinga sera za hali ya hewa Australia


Watu wakiandamana huko Sydney Australia kupinga sera za serikali za hali ya hewa na mikakati iliyotoa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa huko Glasgow Jumamosi Novemba 6,2021.
Watu wakiandamana huko Sydney Australia kupinga sera za serikali za hali ya hewa na mikakati iliyotoa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa huko Glasgow Jumamosi Novemba 6,2021.

Zaidi ya watu 1,000 waliandamana siku ya Jumamosi katika miji mikubwa ya Australia ya Sydney na Melbourne kupinga sera za serikali za hali ya hewa na mikakati iliyotoa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa huko Glasgow.

Haya yakiwa maandamano ya kwanza ya kisheria ya Sydney baada ya kufungwa kwa miezi kadhaa kutokana na masharti ya COVID-19 yalishuhudia takriban watu 1,000 wakiandamana kuunga mkono siku ya kimataifa ya haki ya hali ya hewa, harakati ya kiulimwengu iliyohamasishwa wakati wa mkutano wa COP26.

"Sote tuko hapa ili kuonyesha kwamba tunataka zaidi kutoka kwa serikali yetu," Mmoja wa waandamanaji aitwaye Georgia, alisema.

Waandamanaji walibeba mabango yenye maandishi, "Tunahitaji mabadiliko ya binadamu, si mabadiliko ya hali ya hewa" na "Code Red for Humanity", katika picha zilizoonyeshwa na vyombo vya habari.

Wiki ya hotuba na ahadi za serikali katika mkutano wa wiki mbili huko Glasgow ilileta ahadi za kumaliza matumizi ya makaa ya mawe, kupunguza uzalishaji wa gesi chafu ya methane na kupunguza ukataji miti.

XS
SM
MD
LG