Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 10:46

Zaidi ya wahamiaji 400 waokolewa baharini


Katika picha hii iliyotolewa na Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, mashua ya mbao iliyojaa kupita kiasi iliyojaa wahamiaji 99 ilisaidiwa na shirika hilo la kibinadamu karibu na pwani ya Libya Novemba 16, 2021.
Katika picha hii iliyotolewa na Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, mashua ya mbao iliyojaa kupita kiasi iliyojaa wahamiaji 99 ilisaidiwa na shirika hilo la kibinadamu karibu na pwani ya Libya Novemba 16, 2021.

Meli ya shirika lisilo la kiserikali la Ujerumani Sea-Watch 3, ikiwa na wahamiaji 444, ilikuwa ikingoja kupewa bandari ya usalama kutia nanga baada ya operesheni  tano za uokoaji kutekelezwa katika Bahari ya Mediteranian.

Meli ya shirika lisilo la kiserikali la Ujerumani Sea-Watch 3, ikiwa na wahamiaji 444, ilikuwa ikingoja kupewa bandari ya usalama ya kutia nanga siku ya Jumanne baada ya operesheni tano za uokoaji kutekelezwa katika Bahari ya Mediteranian.

Siku ya Krismasi , wafanyakazi wa meli hiyo waliwaokoa wahamiaji 257 kutoka kwenye boti za mbao zilizojaa katika eneo la operesheni katika maji ya kimataifa kwenye pwani ya Libya.

Mapema asubuhi ya mkesha wa Krismasi waokoaji waliwaokoa watu 93 wakiwemo watoto wengi waliokuwa peke yao kutoka kwenye mashua ya mbao iliyokuwa hatarini katika maji ya kimataifa kusini mwa kisiwa cha Italia cha Lampedusa.

Wiki iliyopita pekee, takriban watu 160 walikufa maji katikati mwa bahari ya Mediteranian walipokuwa wakijaribu kukimbia, kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

XS
SM
MD
LG