Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 04:01

Zaidi ya Polisi 10 wauwawa kutokana na shambulizi baya la majambazi Pakistani


Maafisa wa usalama wakifanya maombi kwenye mazishi kwa polisi waliouawa katika shambulio la magenge ya wahalifu katika wilaya ya Rahim Yar Khan katika jimbo la Punjab Agosti 23, 2024.
Maafisa wa usalama wakifanya maombi kwenye mazishi kwa polisi waliouawa katika shambulio la magenge ya wahalifu katika wilaya ya Rahim Yar Khan katika jimbo la Punjab Agosti 23, 2024.

Idadi ya vifo kutokana na shambulio baya zaidi la majambazi nchini Pakistani dhidi ya polisi iliongezeka hadi 12 baada ya mmoja wa maafisa aliyejeruhiwa kufariki katika hospitali moja katika jimbo la  mashariki la Punjab, maafisa walisema Ijumaa.

Shambulio la Alhamisi la bunduki na maguruneti ya kurushwa kwa roketi pia liliwajeruhi maafisa wanane. Lilifanyika katika eneo la Kacha katika wilaya ya Rahim Yar Khan, ambalo linajulikana kwa maficho kando ya Mto Indus ambapo mamia ya majambazi wenye silaha nzito huwakwepa polisi.

Mkuu wa polisi wa Punjab Usman Anwar alisema polisi walimuua kiongozi wa majambazi ambaye alikuwa akihusika na shambulio hilo. Katika taarifa yake, alisema operesheni dhidi ya majambazi hao bado inaendelea, na itaendelea hadi jambazi wa mwisho atakapoondolewa mkoani humo.

Forum

XS
SM
MD
LG