Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 09:10

Kauli ya Trump yazua gumzo mitandaoni


Alama za mitandao ya kijamii
Alama za mitandao ya kijamii

Ripoti kwamba rais Mteule wa Marekani Donald Trump alisema angefuta ombi la ununuzi wa ndege mpya za Air Force One ambazo hutumiwa na marais wa Marekani, Jumatano ziliendelea kuzua gumzo mitandaoni kwa siku ya pili mfululizo.

Wiki sita kabla yake kuingia madarakani, aliandika maneno yafuatayo kwenye Twitter: "Boeing wanaunda ndege mpya aina ya 747 Air Force One, za kutumiwa na marais siku zijazo, lakini gharama yake imezidi, zaidi ya $4 bilioni. Futa oda hiyo!"

Kuhusiana na hilo, Moses Muga aliandika kwa Instagram: Huyu kaka hataki mchezo. Ananikumbusha rais mmoja wan nchi fulani ya Afrika Mashariki. Wamarekani mmepata prefect asiyetaka michezo na hela za umma. Mimi napenda jinsi Trump anavyotekeleza kazi zake.

Mtu akisoma yaliyomo kwenye mitandao ya kijamii (AP Photo/Karly Domb Sadof, File)
Mtu akisoma yaliyomo kwenye mitandao ya kijamii (AP Photo/Karly Domb Sadof, File)

Merti Rawlings kwenye Twitter naye aliandika: Huyu rais mteule anapenda sana kujionyesha na kujigamba. Ikiwa Serikali ya Obama iliingia kwenye mkataba na kampuni ya Boeing wa kuundwa kwa ndege mbili au zaidi za kuwabeba marais, mbona Trump analeta kifua mbele, na ili hali hata hajawa rais?

"Mimi nadhani hapendi ndege hizo zinunuliwe kwa sababu hatafaidika nazo. Zinatarajiwa kukamilika na kuanza kutumiwa mwaka 2024, wakati ambapo atakuwa ashaondoka mamlakani, Hawezi kufurahia kwa sababu anapenda maisha ya starehe na anaona vibaya mtu mwingine akitumia ndege hizo," ameandika Ofwono Oneke.

Wanaomkashfu Trump hawaelewi alichokimaanisha kupitia kwa tweet yake. Anavyosema ni kwamba dola bilioni 4 ni nyingi mno na wanafaa kupunguza gharama hiyo. Huyo ndiye kiongozi anayehitajika na Marekani.

Swala lingine linaloendelea kuvuma ni kuhusu zoezi la upigaji kura huko nchini Ghana. Maelfu ya wapiga kura nchini Ghana waliripotiwa kuonekana wakipiga foleni ndefu kwenye vituo vya kupigia kura siku ya Jumatano ili kumchagua rais na wabunge wapya katika uchaguzi mkuu, huku kukiwa na ushindani mkubwa kati ya Rais John Mahama na mwanasiasa maarufu, Nana Akufo Addo.

Kwenye mitandao, Rais Mahama mwenyewe aliandika: "Nataka kukamilisha sera yangu ya uchumi na miundombinu. Kauli hiyo ya Mahama kwenye mitandao ya kijamii imevuta maoni mengi hususan kutoka kwa raia wa Ghana."

Lakini mgombea wa chama kikuu cha upinzani, Nana Akufo-Addo, amemtaja Mahama kama aliyeshindwa na kazi ya kuongoiza taifa la Ghana. Oke Efe anasema kwenye Facebook: Tunahitaji uongozi mpya.

XS
SM
MD
LG