Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 19:44

Wole Soyinka aamua kurudi Nigeria baada ya ushindi wa Trump


Mwandishi Wole Soyinka.
Mwandishi Wole Soyinka.

Mshindi wa tuzo ya Nobel mwenye asili ya Nigeria Wole Soyinka amesema Alhamisi kuwa ametimiza ahadi yake ya kutupilia mbali stakabadhi yake ya kuishi Marekani.

Mshindi wa tuzo ya Nobel mwenye asili ya Nigeria Wole Soyinka amesema Alhamisi kuwa ametimiza ahadi yake ya kutupilia mbali hati yake ya kuishi Marekani, maarufu kama Green Card iwapo Donald Trump angeshinda kwenye uchaguzi wa Urais.

Kabla ya upigaji kura kwenye uchaguzi wa Marekani uliopita,Soyinka alikuwa ameapa kuwa angerudisha "Green Card" yake Marekani iwapo Trump angeshinda kama njia ya kulalamikia kampeni yake kali dhidi ya wahamiaji.

"Green Card" ni kadi ya ukazi wa kudumu ambayo raia wa nje wanapata ili kuweza kuishi Marekani na kuwa na haki nyingi isipokuwa kushiriki katika upigaji kura/

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP Soyinka alisema Alhamisi kuwa tayari amechukua hatua hiyo na kwamba sasa ataendelea tu kuishi nyumbani Nigeria.

Soyinka amekuwa mwandishi maarufu wa vitabu vya michezo ya kuigiza, vitabu vingine pamoja na mashairi na aliweza kushinda tuzo ya Nobel ya fasihi mwaka wa 1996. Amekuwa mhadhiri wa kawaida kwenye vyuo vikuu vya Harvard, Cornell na Yale hapa Marekani.

XS
SM
MD
LG