Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 17:23

WHO yasema ni mapema sana kuondoa tahadhari ya hali ya juu zaidi ya COVID-19


Mkuu wa shirika la Afya Ulimwenguni Tedros Adhanom Ghebreyesus akitoa taarifa juu ya chanjo ya ugonjwa wa homa ya corona (COVID-19).REUTERS
Mkuu wa shirika la Afya Ulimwenguni Tedros Adhanom Ghebreyesus akitoa taarifa juu ya chanjo ya ugonjwa wa homa ya corona (COVID-19).REUTERS

Shirika la Afya Ulimwenguni-WHO lilisema Jumatano ni mapema sana kuondoa tahadhari ya hali ya juu zaidi ya janga la COVID-19, huku janga hilo likisalia kuwa dharura ya kiafya ulimwenguni licha ya maendeleo ya hivi karibuni.

Kamati ya dharura ya WHO kuhusu COVID-19 ilikutana wiki iliyopita na kuhitimisha kuwa janga hilo bado linajumuisha Dharura ya Afya ya Umma ya wasiwasi wa Kimataifa (PHEIC), hali ambayo ilitangaza Januari 2020.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwaambia waandishi wa habari Jumatano kwamba alikubaliana na ushauri wa kamati hiyo.

Kamati hiyo ilisisitiza haja ya kuimarisha ufuatiliaji na kupanua upatikanaji wa vipimo, matibabu na chanjo kwa wale walio katika hatari zaidi, alisema, akizungumza kutoka kwenye makao makuu ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa huko Geneva.

XS
SM
MD
LG