“Tunajua jinsi ya kudhibiti mpox, na ukanda wa Ulaya, zinahitajika juhudi kukomesha maambukizi,” Dkt Hans Kluge, mkurugenzi wa kanda ya Ulaya ya WHO, amewaambia wanahabari Jumanne mjini Geneva.
Amesema miaka miwili iliyopita mpox ilidhibitiwa Ulaya, kutokana na ushirikiano wa moja kwa moja na jumuiya zilizoathirika zaidi za wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja baada ya kufanya uchunguzi wa kina pamoja kutoa ushauri mzuri wa afya ya umma.
Akizungumza kwa njia ya video kutoka Copenhagen, Kluge amesema WHO iliweza kudhibiti mlipuko huo kupitia mabadiliko ya tabia na hatua zisizo za kibaguzi za afya ya umma, pamoja na chanjo ya mpox.
Forum