Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 01, 2025 Local time: 20:27

WHO yaorodhesha michezo ya Kompyuta kama 'ugonjwa'


Mtu akicheza Computer game
Mtu akicheza Computer game

Shirika la afya duniani (WHO) limeorodhesha michezo ya video yani video games kama ambayo inachangia ugonjwa wa akili. Katika ripoti iliyotolewa Jumatatu, WHO ilisema kuwa hali hii inaathiri asili mia tatu ya wachezaji wa michezo hiyo.

WHO imesema baadhi ya watu hucheza video games bila hata kufikiria, jambo ambalo linawafanya wategemee sana michezo hiyo. Wengine huachana na shughuli zao za kawaida ili kucheza michezo hiyo, kwani wasipofanya hivyo, huonekana wanyonge wadhaifu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, Zaidi ya watu bilioni mbili duniani wanacheza michezo hiyo.

Shirika hilo limesema kwamba sababu ya kuorodhesha michezo hiyo ya video games kama inayochangia ugonjwa wa akili ni kuhamasisha watu kuhusu hatari ya kutegemea sana michezo hiyo.

Tayari kuna kituo cha matibabu mjini Los Aneles, California, ambacho kinawahudumia watu walio na hali hiyo ya kuzoea video games kiasi kwamba ni vigumu kuachana nazo.

Christoper Malian, mhasisi wa kituo hicho amesema kwamba vijana ndio walioathiriwa sana na hali hii.

"Tunawahudumia watoto wa umri wa chini hata kuanzia miaka mitano, hata wakati wa ujana wao ujana wao, hadi wakiwa watu wazima," alisema Malian.

Aliongeza kuwa changamoto kubwa, hata baada ya waathiriwa kutibiwa katika kituo hicho, ni kwamba wakiondoka, wanaendelea kutumia vifaa vya mawasiliano kama simu, ambavyo vinachangia pakubwa kwa watu kuzoea michezo hiyo.

WHO inaonya kwamba iwapo vijana hawatapunguza mazoea ya kucheza video games, hali hii huenda ikazorota na kuwaona hata watu wengi Zaidi wakitafuta matibabu kwa sababu ya kile ambacho sasa kimeorodheshwa kama ugonjwa wa akili na shirika hilo.

XS
SM
MD
LG